Biashara nyingi huwekeza kwa kiwango kikubwa katika ununuzi wa mitambo inayokidhi mahitaji yao mahususi. Hata hivyo, mitambo hii inaweza kukumbwa na hitilafu zisizotarajiwa katika matumizi yake. Bima ya Uharibifu wa Mitambo hutoa kinga dhidi ya uharibifu wa mitambo hiyo, ikijumuisha gharama za usafishaji, ukaguzi, kuvunja na kutengeneza upya, pamoja na kuiondoa eneo ilipo.
Bima hii inafidia uharibifu au hasara ya ghafla na isiyotarajiwa inayotokea kwa bahati mbaya, isipokuwa kwa yale yaliyozuiwa na masharti ya bima. Mifano ya mitambo inayoweza kulindwa na bimah hii ni pamoja na lifti, jenereta, vinu vya kupandishia watu au mizigo (elevators na escalators), na mitambo ya viwandani.
Wigo wa Bima ya Uharibifu wa Mitambo:
Sera ya Kawaida ya Bima ya Mitambo hutoa ulinzi dhidi ya uharibifu wa ghafla na usiotarajiwa wa mali iliyowekewa bima, kutoka kwa sababu yoyote ile (isipokuwa hatari zilizoondolewa na mkataba). Uharibifu huo unaweza kutokea katika hali zifuatazo:
Chanzo cha Matukio Yanaweza Kuwa: