WADAU SEKTA YA BIMA MNAKUMBUSHWA KUCHUKUA TAHADHARI MABADILIKO YA HALI YA HEWA NCHINI JUNI - AGOSTI 2025
- Iliwekwa 01-08-2025
TMA watoa tahadhari, wadau sekta ya bima tafadhali chukua tahadhari za hali ya hewa nchini.
TMA watoa tahadhari, wadau sekta ya bima tafadhali chukua tahadhari za hali ya hewa nchini.
Zanzibar, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) kwa kushirikiana na wadau wake ambao ni TAN – RE na ATI leo jumatatu Julai 28, 2025 wamefanikisha mafunzo rasmi yahusuyo bima ya Takaful kwa watoa huduma hiyo, katika bima visiwani humo. Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali.
Dodoma, Juni 2025 – Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, ambayo inalenga kuiwezesha nchi kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa misingi ya usawa, ubunifu, na ushindani wa kidijitali. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma, ukihudhuriwa na viongozi wa serikali, sekta binafsi, mashirika ya kiraia na washirika wa maendeleo.
Kampuni za Bumaco Insurance Co. Ltd na Bumaco Life Insurance zimeshiriki kikamilifu katika Uzinduzi wa Kijiji cha Bima, uliofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 4 Julai 2025, katika Viwanja vya Saba Saba – Kijiji cha Bima, kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi 5:30 asubuhi.
Katika maadhimisho ya Insurance Day yaliyofanyika jijini Arusha jana Ijumaa tarehe 20 Juni 2025, kampuni ya Bumaco ilitunukiwa tuzo ya heshima kwenye Hall of Fame, tuzo ya heshima kutoka (IIT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).