BUMACO YAPATA TUZO YA HESHIMA KWENYE INSURANCE DAY 2025.

BUMACO YAPATA TUZO YA HESHIMA KWENYE INSURANCE DAY 2025.

  • Date 21-06-2025

Arusha, Ijumaa - Juni 20, 2025

Katika maadhimisho ya Insurance Day yaliyofanyika jijini Arusha jana Ijumaa tarehe 20 Juni 2025, kampuni ya Bumaco ilitunukiwa tuzo ya heshima kwenye Hall of Fame, tuzo ya heshima kutoka (IIT) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA).

Tuzo hii maalum ilitolewa kwa kutambua mafanikio ya Bumaco kama kampuni ya kizalendo iliyoanza safari yake kama wakala wa bima na hatimaye kukua hadi kuwa kampuni kamili ya bima.

Tuzo hiyo ilipokelewa kwa niaba ya wanahisa, bodi ya wakurugenzi, na kampuni kwa ujumla na Dr. Rogathe Mshana, ambaye alitoa shukrani kwa niaba ya Bumaco na kuahidi kuendeleza ubora katika utoaji wa huduma za bima nchini.

Tukio hili limeendelea kuonesha mchango mkubwa wa kampuni za kizalendo katika ukuaji wa sekta ya bima Tanzania.

HUDUMA ZA BIMA ZENYE UHAKIKA