Bima hii ni mahsusi kwa ajili ya nyumba za kuishi pamoja na mali binafsi inayoweza kuhamishwa.

Mali zinazolindwa na Bima hii ni pamoja na:

  • Majengo ya makazi
  • Vifaa vya kielektroniki kama vile kompyuta, kamera, televisheni, redio, n.k.
  • Samani kama viti, meza, makabati, na kadhalika

Hasara Zinazolipiwa Fidia Zinajumuisha:

  • Moto
  • Wizi
  • Mafuriko
  • Matetemeko ya ardhi.
  • Ajali mbalimbali, kama kugongwa na mti ulioanguka au gari lililotoka barabarani, n.k.

Ada ya Bima

Kiwango cha ada ya bima ya nyumba na mali hutegemea thamani ya mali kama ilivyokadiriwa mwanzoni mwa mkataba. Mkataba unaweza kubadilishwa ili kuakisi mabadiliko ya thamani ya nyumba au mali binafsi kila wakati mkataba wa bima unapohuishwa.