Bima hii hutoa kinga dhidi ya hasara ya kifedha itakayotokea kutokana na uporaji au wizi wakati wa usafirishaji wa fedha au ikiwa fedha hizo ziko katika majengo ya biashara. Bima hii hufidia fedha zinazobebwa na mhusika wa mkataba wa bima au wafanyakazi waliidhinishwa, pamoja na fedha ambazo hazijatolewa na zimehifadhiwa kwenye sanduku la usalama. Hii inajumuisha fedha taslimu, noti za fedha, hati za hazina, hundi, maagizo ya posta, na stempu halali za posta. Biashara zinahitaji kuwa na bima ya kwa ajili ya kulinda fedha zao.
Wigo wa Bima ya Fedha:
- Hasara ya fedha wakati wa usafirishaji, inayofanywa na mteja aliyekata bima au mfanyakazi aliyeidhinishwa, kutokana na uporaji, wizi, au sababu nyingine zisizotarajiwa.
- Uwajibikaji wa kampuni ya bima kwa tukio la hasara ya fedha zilizo katika sanduku salama la kuhifadhia fedha, kutokana na wizi wa kuvunja, kuvunja nyumba, uporaji, au kushambuliwa, utazingatia kiwango cha juu kilichobainishwa kwenye mkataba wa bima.
- Hasara ya fedha zinazotokea wakati wa saa za kazi au baada ya saa za kazi.
- Uharibifu wa sanduku la kuhifadhia fedha au kifaa kinachotumika kuhifadhi fedha, ambapo thamani ya kifaa hicho inaweza kulipwa iwapo uharibifu utatokea.
- Hasara ya fedha zilizokuwa chini ya uangalizi wa mfanyakazi aliyeidhinishwa, kwa masharti kuwa uidhinishaji huo umetambuliwa na kukubalika na kampuni ya bima.