Bima ya Moto

Bima ya Moto ni bima inayomlinda mteja dhidi ya hasara zinazotokana na majanga ya moto. Majanga ya moto yanaweza kutokea wakati wowote, na yanapotokea, husababisha kubwa kwa mali na biashara.

Bima hii inaweza kukatwa kwa ajili ya majengo kama vile:

  • Nyumba za makazi

  • Nyumba za biashara

  • Maghala ya kuhifadhi bidhaa mbalimbali, n.k.

Iwapo majanga ya moto yakitokea, Bima hii itatoa fidia inayolingana na thamani ya jengo lililoungua. Ukiwa na Bima ya Moto, unakuwa na utulivu wa akili kuhusu suala la hasara unayoweza kupata kutokana na janga la moto.

Ada ya bima hulipwa kwa kipindi cha mwaka mmoja.