Kampuni za Bumaco
Insurance Co. Ltd na Bumaco Life Insurance zimeshiriki kikamilifu
katika Uzinduzi wa Kijiji cha Bima, uliofanyika siku ya Ijumaa,
tarehe 4 Julai 2025, katika Viwanja vya Saba Saba – Kijiji cha Bima,
kuanzia saa 3:30 asubuhi hadi 5:30 asubuhi.
Tukio hilo la kitaifa
limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya bima nchini, likiongozwa na Kamishna
wa Bima Tanzania, Dkt. Baghayo Saqware, ambaye alitoa hotuba ya uzinduzi
akisisitiza umuhimu wa elimu ya bima kwa wananchi na nafasi ya sekta hiyo
katika kukuza uchumi.
Kupitia banda lao maalum,
Bumaco ilitoa elimu kwa wananchi kuhusu huduma mbalimbali za bima.
Ushiriki wa Bumaco katika
tukio hili ni ushahidi wa dhati wa dhamira yao ya kuendelea kusogeza huduma
karibu na wananchi, kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa bima, na kuchangia
katika ujenzi wa jamii yenye kinga ya kifedha dhidi ya majanga.