Mwanza, Juni 2025: Kampuni ya Bumaco Insurance pamoja na Bumaco Life Assurance zimeshiriki kikamilifu katika Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, lililoandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo. Kampuni ya Bumaco Insurance pamoja na Bumaco Life Assurance zimeshiriki kikamilifu katika Jukwaa la Nne la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini, lililoandaliwa na Wizara ya Madini kwa kushirikiana na wadau wa sekta hiyo. Jukwaa hili limefanyika jijini Mwanza na limewakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wachimbaji wa madini, wawekezaji, wakandarasi, taasisi za kifedha na mashirika ya bima.
Kupitia ushiriki wao, Bumaco Insurance na Bumaco Life waliweza kuonesha mchango mkubwa wa sekta ya bima katika kuimarisha shughuli za madini kwa kutoa elimu juu ya bidhaa na huduma zinazolenga kupunguza hatari na kuongeza usalama wa shughuli za migodini. Banda la Bumaco lilitembelewa na wadau mbalimbali waliopata maelezo kuhusu huduma za:
Bima ya magari na mitambo ya migodini
Bima ya majanga kwa mitambo na mali
Bima ya maisha kwa wafanyakazi wa migodini
Bima ya ajali za binafsi kwa wachimbaji
Wataalam wa kampuni walishiriki pia katika mijadala ya kitaalamu, wakitoa mada na maelezo kuhusu umuhimu wa kuwa na kinga ya kifedha dhidi ya majanga yasiyotabirika. Bumaco ilisisitiza kuwa bima si gharama bali ni uwekezaji katika usalama na ustawi wa sekta ya madini.
Mmoja wa Wataalam wa Masoko Bumaco alinukuliwa akisema: "Kwa maendeleo endelevu ya sekta ya madini, ni muhimu kuwa na mifumo madhubuti ya usimamizi wa hatari na kinga ya kifedha. Bima sio gharama – ni uwekezaji."
Kwa kupitia jukwaa hili, Bumaco pia imepata fursa ya kuimarisha mahusiano na wadau wapya na wa muda mrefu, ikiwa ni pamoja na kampuni za uchimbaji, wasambazaji wa vifaa, mashirika ya serikali na binafsi, na wachimbaji wadogo.
Bumaco Insurance na Bumaco Life zitaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono jitihada za serikali na sekta binafsi katika kuhakikisha Watanzania wananufaika ipasavyo na rasilimali za taifa kupitia kinga madhubuti za bima.