Arusha, Juni 19, 2025 – Kampuni za bima Bumaco Insurance na Bumaco Life leo zimethibitisha tena dhamira yao ya kujihusisha na afya ya jamii na kukuza elimu ya bima kwa kushiriki kikamilifu kwenye tukio la Bima Walk, lililofanyika jijini Arusha.
Tukio hilo lililojumuisha matembezi ya hiari (walk for awareness), lililenga kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na bima katika maisha yao ya kila siku—ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya bima nchini. Bima Walk ni jukwaa ambalo hukutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya bima, wakiwemo watoa huduma, wateja na wadau wa maendeleo, kwa lengo la kujenga uelewa na kuimarisha mahusiano baina ya sekta hiyo na jamii.
Bumaco Insurance na Bumaco Life, zikiwa miongoni mwa kampuni zinazotoa huduma bunifu za bima nchini, ziliungana na mashirika mengine katika kuonyesha mshikamano na kujitolea kwao katika kuimarisha afya ya jamii na kutoa elimu kuhusu bidhaa mbalimbali za bima, zikiwemo bima ya afya, maisha, magari na biashara.
Kupitia ushiriki wao katika Bima Walk, kampuni hizi zimeendelea kuonesha kuwa bima si tu huduma ya kifedha bali pia ni nyenzo ya kijamii inayowezesha ustawi wa watu, familia na biashara.
HUDUMA ZA BIMA ZENYE UHAKIKA