Dar es Salaam, Juni 20, 2025 – Kampuni za bima Bumaco Insurance na Bumaco Life zimejitokeza kama miongoni mwa wadhamini wakuu wa tamasha maalum la kiroho na kijamii lijulikanalo kama Twen’zetu kwa Yesu 2025 – Corporate, lililofanyika tarehe 19 Juni 2025 katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Tamasha hilo lilikusanya maelfu ya washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini, likiwa na lengo la kuhamasisha mshikamano wa kiimani , wakurugenzi, wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi.
Tamasha la Twen’zetu kwa Yesu 2025 – Corporate limeonesha kuwa jukwaa bora la kuwakutanisha viongozi wa sekta mbalimbali na kuwapa nafasi ya kushiriki ibada na tafakari ya pamoja, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika jamii kupitia imani, mshikamano, na maadili.
HUDUMA ZA BIMA ZENYE UHAKIKA