Bima hii ni mahususi kwa ajili ya Nyumba za makazi na mali za ndani zinazohamishika

Mali zinazopata kinga ya Bima hii ni pamoja na:-

  • Jengo
  • Vifaa vya kielektroniki kama kompyuta/ kamera/ TV/ redio nk
  • Samani: kama vile viti/ meza/ kabati/ nk

Hasara zinazofidiwa ni zile zitokanazo na majanga kama:-

  • Moto
  • Wizi
  • Mafuriko
  • Tetemeko la ardhi
  • Ajali kama kuangukiwa na mti/ gari iliyoacha njia nk

Mkataba wa Bima hii ni wa mwaka mmoja

Ada/tozo za Bima ya Nyumba na Mali, hutegemea thamani ya ukadiriaji na tathmini inayofanyika mwanzoni mwa mkataba. Mkatabima huweza kurekebisha taarifa za thamani ya nyumba au mali za ndani, kila anapohuisha Mkataba wake wa Bima